CHANGAMOTO SITA AMBAZO KILA MJASIRIAMALI ATAKUTANA NAZO
Labda unawaza kuhusu kujikita katika ujasiriamali katika muda huu. Pengine tayari wewe ni mjasiriamali tayari mwenye biashara moja au zaidi. Katika mtihani wale waliosoma vitu vilivyotolewa katika mtihani ndio ambao wana uwezekano mkubwa wa kufaulu mtihani huo. Vivyo hivyo katika jambo lolote maishani. Tutaangalia changamoto unazoweza kukutana nazo kama mjasiriamali ili uweze kujiandaa vizuri kuzishinda pale utapokutana nazo.
1. CHANGAMOTO YA KUKUBALI KUACHANA NA MSHAHARA
Kuna amani kubwa sana moyoni pale unapojua kuwa kila tarehe 30 shilingi laki kadhaa au milioni kadhaa zitatua katika akaunti yako ya mshahara. Kwa wengi mshahara unafanya uepuke mawazo ya shida za kipesa kwa sababu unajua kuwa kila tarehe flani nitapata kiasi flani. Ni hali ambayo inaweza kuzoeleka kirahisi sana na kumfanya mtu aogope kuuacha pale atapoamua kujiingiza katika ujasiriamali kwa muda wote. Inabidi ujiandae na hili toka siku ya kwanza unayoanza ujasiriamali. Kuwa na akiba kutasaidia kuondoa mawazo ya shida za kipesa iwapo itabidi uache kazi ili kujiingiza katika ujasiriamali full time.

2. CHANGAMOTO YA KUSIMAMIA MTAJI
Jinsi unavyotumia mtaji wako kunaweza kufanya biashara yako ifanikiwe au ishindwe. Iwapo utatumia mtaji kwa matumizi yasio ya lazima basi mtaji wako utaisha haraka na kuna uwezekano mkubwa biashara yako haitadumu zaidi ya miezi sita. Lakini jambo lingine la kuangalia ni kuwa kwa kawaida vitu ulivyodhani vitagharimu kiasi flani huenda vikagharimu zaidi. Ile bajaji uliyodhani itakugharimu milioni 6 kumbe inahitaji insurance na vibali vingine ambavyo vitagharimu laki 2 ya ziada kila mwaka. Ile ofisi uliyodhani itakugharimu laki 5 kwa mwezi kumbe kuna ada ya usafi ya shilingi elfu 30 kila mwezi. Kufanya maamuzi sahihi ya katika kutumia mtaji wako utavyokutana na vitu kama hivi kutakufanya ufanikiwe.

3. KUSIMAMIA ISHU ZA KIBIASHARA
Hapo juu nimeongelea kuhusu kusimamia mtaji ila kuna mambo mengine mengi yanaweza kutokea katika biashara yako. Vitu kama mmoja wa wafanyakazi wako kuchelewa kazini mara kwa mara, au labda benki kufungwa kabla ya wewe kukamilisha muamala muhimu na hata kukuta kuwa bidhaa zinakudodea wakati ulidhani zitauzika haraka. Kuna ishu nyingi sana za kibiashara ambazo zinaweza kukuletea changamoto. Jinsi utavyosimamia mambo katika changamoto hizi aidha kutakufanya ufanikiwe au usifanikiwe. Ni muhimu sana kuwa na akili iliyotulia ili kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya biashara yako.

4. UPWEKE
Kama mjasiriamali, upweke ni moja kati ya vitu ambavyo utakutana navyo katika safari yako kuelekea mafanikio na pengine hata utapofanikiwa. Itafika siku utakuta mambo hayaendi unavyotaka na huna wa kumpigia kumlalamikia. Unaweza usiweze kutafuta ndugu na marafiki kwa sababu walikuambia usijiingize katika ujasiriamali. Hivyo ukiwapigia katika wakati huo wa shida huenda ukaonekana unakata tamaa. Pia katika siku nyingi utajikuta upo ofisini peke yako mpaka usiku wa manane kukiwa hamna mtu wa kukuletea hata kahawa kukuzuia usilale. Hakuna kuchekacheka na watoto, kuteta na marafiki ama kujiliwaza na mama watoto. Ni wewe na kazi tu. Ni vema ukajua hili mapema kwa sababu kwa wengi jambo hili huwafanya wakate tamaa, hususani kama katika wakati huo wanaandamwa na matatizo katika biashara zao pia. Cha muhimu kuzingatia ni kuendelea kusonga mbele na utafika malengo yako.

5. CHANGAMOTO YA KUFANYA VITU VINGI KATIKA WAKATI MMOJA
Hususani kama mjasiriamali unayeanza, kuna kipindi itabidi uwe unahusika kutenda vitu vingi katika biashara yako. Wewe unaweza ukawa ndie unauza vitu dukani kwako. Wewe huyohuyo unaweza ukawa ndie unaepost bidhaa zako katika Instagram. Wewe huyohuyo unaweza ukawa ndie unaepokea simu zote zinazoingia katika biashara yako. Kabla hujaanza kuajiri watu wakusaidie basi utakuwa na majukumu mengi. Changamoto inakuja kwenye jinsi ya kuyafanyia kazi majukumu hayo vizuri ili biashara yako iendelee kukua. Na hapa ndipo umuhimu wa kuwa tayari kujifunza unapoingia. Hutajua kila kitu hivyo ni vema ukajitahidi kutafuta wale wanaojua vitu flani wakufundishe. Yote haya ni muhimu ili kuhakikisha unafanikiwa.

6. KUBADILIKA KWA MFUMO WA MAISHA
Iwapo wewe ratiba yako ya wikiendi ni ya viwanja basi ukishaanza ujasiriamali hili litabadilika. Kuna watu ratiba zao ni kuwa Alhamisi ni kuzuka Ladies Night club, Ijumaa na Jumamosi disco kisha Jumapili mchana hadi saa 4 usiku kijiweni na washkaji wakipata moja moto moja baridi huku wakipiga soga za hapa na pale. Hata kama huyu sio wewe kwa asilimia mia moja, ni vema ukatambua kuwa utapoanza ujasiriamali basi muda wako mwingi utatumika katika biashara yako na si kwenye starehe. Itabidi uanze kukataa mialiko ya kwenda kula bata na washkaji. Itabidi matumizi yako ya pesa yaelekee katika kuikuza biashara yako na si kwingineko. Na pia mara nyingi itabidi ubadilishe kabisa marafiki zako uwe na wale ambao hawatakurudisha nyuma katika safari yako ya ujasiriamali. Na hapa ndipo wengi wanapogonga mwamba. Wao wanataka mafanikio katika ujasiriamali huku wakiendelea na starehe. Ukweli ni kwamba hakuna aliyefika mafanikio makubwa kwa namna hiyo. Hivyo ni vema ukafanya maamuzi ya nini unataka katika maisha yako iwe bata au mafanikio katika ujasiriamali. Iwapo ni ujasiriamali basi jiandae kubadilisha mfumo wako wa maisha ili ufikie mafanikio.

Nimetumia neno changamoto katika makala hii badala ya matatizo kwa makusudi. Nataka kukuonesha kuwa unaweza kuvishinda vitu hivi vitakapotokea katika safari yako kuelekea mafanikio. Hivi ni vitu vya mpito. Utapokutana nazo basi usikate tamaa. Endelea kukaza mwendo mpaka utapofikia ndoto zako.
Imeandikwa na:
SIMON MNYELE
SIMON MNYELE
ConversionConversion EmoticonEmoticon