Mafanikio yoyote yana hatua ambazo mhusika hupita, hatua hizo ndiyo unifanya kusema, “mafanikio ni mchakato, na sio tukio la usiku mmoja”. Zipo hatua kadhaa ambazo lazima upitie ili kufanikisha kusudi lako. Kama hujui hatua hizi za mafanikio, tafadhali pitia andiko hili kwa kubofya hapa.
Hatua ya kwanza kabisa katika mafanikio ya kitu chochote ni kutamani, kutamani huja kwa kujua hasa ni nini unachokitaka katika maisha yako, hivyo ule msukumo wa ndani ndiyo tunauita ‘tamaa’. Ni vingumu kutamani kama hujui nini hasa unachokitaka katika maisha yako.
Kutamani ndiyo hatua ya awali kabisa kuelekea utajiri. Huwezi kuwa tajiri kama hujatamani kwanza kuwa tajiri. Ndiyo maana mara zote huwa nasema kwamba kuwa tajiri au maskini ni chaguo lako. Unapochagua kwa dhati kuwa tajiri hakika utaanza kusaka maarifa ya mbinu za kuwa tajiri kwa shauku kubwa ndani yako na hatimaye utakuwa.
Hayupo wa kukuzuia; si serikali, si wazazi, wala marafiki. Hatima yako ipo mikononi mwako. Unapoamua kuwa tajiri na ukasukumwa na tamaa inayowaka ndani yako kama moto hakika unapata nguvu kubwa ya kuhakikisha unaupata utajiri katika mikono yako. Tamaa ni nguvu ambayo ikitumiwa huleta shauku ya kufika kwenye hatima bora.
“Wewe ni mkuu wa hatima yako na kiongozi wa nafsi yako kwa sababu una nguvu ya kusimamia fikra zako”
Utafanikiwa maishani ikiwa tu utachagua lengo la uhakika, sambamba na kuelekeza nguvu, juhudi zote na kila kitu kuunga mkono lengo lako. Unapokuwa kwenye lengo la uhakika ni sawa na kuwa katika njia sahihi ya ndoto zako. Hii itakusaidia kuchochea moto wa matamanio yako mpaka uifikie hatima yako. Hivyo ipo haja ya kuchagua vyema lengo/kusudi lako ambalo halipingani na mapenzi ya moyo wako.
Washindi ni wale walioamua kwa dhati bila kugeuka na kusonga mbele bila kukoma. Na maamuzi yao yakashikiliwa wakati wote na akili zao. Ni wazi akili ni rasilimali muhimu sana katika kukamilisha matamanio yako. Ni lazima akili yako kila mara ijenge picha ya kule utakapo kufika, lazima uuone utajiri huu unaoutaka hata kama haujaufikia bado; yawezekana ikawa ngumu lakini itakubidi ujizoeze tu.
Kutaka tu, hakutoshi kuleta mafanikio au utajiri maishani, bali kutamani kukiungwa mkono na mpango kazi na kudumu kutekeleza mpango huo mpaka utakapokuwa kitu halisi. Hivyo ni kusema baada ya kutamani ni lazima uandae mpango kazi wa kukufikisha huko na hatimaye uufanyie kazi ule mpango kazi mpaka ukuletee matunda. Kumbuka hakuna kitu cha bure, kila kitu kina gharama zake.
Zifuatazo ni njia sita (6) ambazo unaweza kuzitumia kugeuza matamanio yako ya kuwa tajiri kuwa utajiri halisi:-
Moja, Amua akilini kiasi cha fedha unachotamani na sio kusema “nataka pesa nyingi”. Akili yetu ina uwezo tu wa kuvuta kitu dhahiri hivyo eleza kiasi mahsusi.
Soma: Moja ya Kosa Kubwa Ambalo Husababisha Kushindwa ni hili Hapa.
Pili, onyesha kwa usahihi ni nini unachokusudia kukifanya au kutoa ili upate hicho kiasi cha pesa unachohitaji. Kumbuka hakuna kitu cha bure. Hapa unapaswa kueleza shughuli ambayo utaifanya ili kukuzalishia hicho kiasi cha pesa utakacho.
Tatu, andika tarehe ambayo unatamani umiliki kiasi hicho cha pesa unachotamani. Achana na usemi wa jumla jumla tu, eleza tarehe mahsusi. Kufanya hivyo utaipa jukumu akili yako ya ndani kutoa jibu katika tarehe husika.
Nne, tengeneza mpango wa kutekeleza matamanio yako. Hakikisha unauanza kuutekeleza mpango huo mara moja baada ya kukamilika, bila kujali upo tayari au la!
Tano, andika kwenye karatasi maelezo mafupi ya kiasi cha pesa utachotaka, na tarehe ambayo unatamani hicho kiasi uwe nacho, eleza huduma, biashara au kazi utakayofanya ambayo ndiyo itakuzalishia kiasi hicho cha pesa unachokitaka kisha eleza mpango utakaoutumia kupata hicho kiasi kwa kutumia sentensi chache.
Sita, Soma andiko lako kwa sauti mara mbili kwa siku. Mara moja asubuhi unapoamka na mara ya pili kabla hujalala. Unaposoma jenga picha akilini na uhisi na uamini kweli unamiliki kiasi hicho cha pesa. Fanya hivyo bila kusita endelea mpaka utakapofanikisha na utashangaa mwenyewe uwezo wa ajabu uliyopo katika mbinu hizo.
MUHIMU: Ikitokea kwa wakati unatumia mbinu hizi kuvuta kiasi cha pesa unachokihitaji huna shughuli au kazi ambayo itakuzalishia kiasi hicho, basi wewe wala usipate shida kabisa, fanya hivi, wewe andika kiasi unachokihitaji, kisha jenga picha akilini unamiliki kiasi hicho na huhisi unakimili tayari, ona kama kiko kwenye uthibiti wako. Unaweza ukawa unahisi unaenda benki kutoa pesa hizo au hisi uko nazo nyumbani unazipangia matumizi n.k. Kwa kufanya hivyo utashangaa uwezo wako wa akili unavyofanya kazi kwani utakuletea mpango wa kupata kiasi hicho kupitia fikra au wazo na utalianza kulifanyia kazi mara moja.
Kumbuka, wote waliofanikisha utajiri, walianza na ndoto akilini mwao, kisha wakatarajia, wakatamani kweli kuwa hivyo na wakapanga mipango kabla ya kupata kiasi hicho cha pesa wanachomiliki. Mbinu hizi zinafanya kazi wa mtu ye yote bila kujali kiwango chake cha elimu alichonacho.
Asante kwa kuongozana nami toka mwanzo hadi mwisho. Nikutakie mafanikio mema katika safari yako. Endelea kuweka juhudi na maarifa katika safari yako na hatimaye muda si mrefu utafanikisha. Usiache kulisha akili yako kwa makala walau moja kwa siku kupitia mtandao huu.
Ni mimi rafiki yako,
Alex Mushi.

ConversionConversion EmoticonEmoticon