Katika safari ya kukua kifikra na kuelekea Hatima ya Mafanikio yetu,Tunahitaji maarifa na Ujuzi unaoendana na kiwango cha kule tunakohitaji kufika,au kile tunahitaji kufanya..
Watu wengi wamejikuta wao wapo katika viwango vya Juu hivyo wakajiona wao wenyewe ndio Maarifa,wao ndio wanapaswa kufundisha na kuangaliwa TUU ndio maana madaraka yao yanaporomoka bila wao kudhani,biashara zao na kampuni zao zinakufa,ndio maana Taasisi na shuguli zao zinawashinda maana watu wa aina hii ni kero hata kwa jamii maana hawapo tayari kujifunza ila eti wafundishe wao..
kuna watu wanaamini kuaminiwa kupewa vyeo na madaraka au kuitwa Baba au Mama basi kila kitu Yeye anajua,kuna mwingine anadhani KUMILIKI Mali nyingi na utajiri hivyo hahitaji maarifa na ujuzi tena ila yeye atoe.
Sikiliza Maarifa na ujuzi unaambatana sana na Hekima Na unyenyekevu, ukitaka kuifikisha taasisi yako,mradi wako, kampuni,kilimo chako,mbali kimafanikio, usiwe MTU wa kujiona umejitoshereza,kimaarifa kila siku,kiuwezo,n.k Bali uwe mtu wa kujishusha,kuhitataji,uwe MTU wa Kujifunza zaidi na ili ujifunze zaidi unahitaji kunyenyekea hata kwa wasio na uwezo kama wewe ila sana maarifa,Jambo linafurahisha na kunifundisha sana ni KUTOKA KWA BILGATE tajiri wa kwanza duniani lakini Likizo yake ya wiki mbili kwa mwaka, Huwa anaitumia Kusoma vitabu vinavyoongeza maarifa take na ujuzi wake ktk kuongoza Kampuni zake,kuongeza ubunifu wa kiuchumi,bidhaa na masoko na vitabu hivyo vinaandikwa na watu wasio kama yeye wapo chini yake kifedha,kiuwezo n.k.
Je, wewe unawezaje kufika mbali bila kujifunza?bila kuongeza ujuzi,maarifa,na bila kujishusha na kunyenyekea kwa ajili ya kujiongezea THAMANI na ubora wa kuifikia Hatima yako?,Neno LA Kingereza UNDERSTOOD maana yake ni kuelewa,ila Tafsiri yake ni Ili uelewe,unahitaji kuwa Chini (under) wakati umesimama(stood) yaani unyenyekee kwa mwenye maarifa,ujishushe,ndipo Utaelewa na kujifunza vizuri,huwezi jifunza kwa kuagalia cheo chako na hali yako halafu ukafananisha na Mwalimu.
#JIFUNZEKUJIFUNZA.
#JIFUNZEKUJIFUNZA.


ConversionConversion EmoticonEmoticon