Sidhani kama kila mtu anataka kuondoka katika hii dunia huku akiacha akaunti zake za kwenye mitandao zikiwa zinatumiwa na jamaa zake au zipo tu zinaelea milele. Kama wewe ni mmoja kati ya hao watu wanaotaka kujiondoa kabisa katika mitandao baada ya kufa, unatakiwa kupanga mipango mapema ya kufuta akaunti zako zote za kwenye mitandao pindi ukiaga dunia.
Baadhi ya mitandao kama Google na Facebook, wanakupa uwezo wa kuweka muda wa kufutika kwa akaunti zako kabla haujafa. Ila mitandao mingine itabakia na akaunti zako milele labda kama ndugu au jamaa wakitaka zifutwe kwa njia ya mahakamani. Leo nitakuonesha jinsi ya kuhakikisha akaunti zako zinafutika pindi tu ukiaga dunia hii na hakuna mtu ambaye atajua chochote kuhusu akaunti zako hizo.
Hakikisha akaunti zako mitandaoni zinafutwa pindi ukifa
Facebook ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo inakupa uwezo wa kurithisha akaunti yako, unaweza ukairithisha akaunti yako kwa jamaa au ndugu ambaye ataisimamia na kutunza taarifa zako pindi ukifa. Facebook pia inakupa uwezo wa kufuta akaunti yako pindi ukifa.
Ili kuhakikisha akaunti yako inafutika pindi ukifa, fungua Facebook kisha nenda kwenye Settings > Security > Legacy Contact. Hapo utachagua rafiki au jamaa ambaye atarithi na kusimamia akaunti yako baada ya wewe kufariki.
![]() |
| Settings > Security > Legacy Contact |
| Andika jina la mtu ambaye atairithi akaunti yako ya facebook |
Au unaweza ukapangilia kufutwa kwa akaunti yako moja kwa moja bila mtu yeyote kuirithi, Facebook wakishapatiwa taarifa juu ya kifo chako basi akaunti yako itafutwa mara moja. Bonyeza hapo kwenye request account deletion utaona kiboxi ibukizi kikitaka ukubali kufutwa kwa akaunti yako pindi ukifariki. Bonyeza Delete After Death.
| Bonyeza Delete After Death |
Google inakipengele cha 'Inactive Account Manager' ambapo kinakuruhusu kuchagua nini kifanyike pindi akaunti yako itakapokuwa haitumiki kwa kipindi cha muda flani. Unaweza ukaipangilia 'Inactive Account Manager' ifute akaunti yako ya Google na huduma zote ilizounganishwa nazo, kuanzia Gmail, Blogger, Adsense pamoja na YouTube.
Ili kupangilia hivi, ingia kwenye akaunti yako ya Google kisha ingia kwenye ukurasa huu hapa. Google wataitaji namba yako ya simu au barua pepe ili kukutahadharisha kabla ya kufutwa akaunti yako, Google watakutumia ujumbe kukutaarifu muda wa kufutwa akaunti yako umefika kwa hiyo utaweza kufahamu na kuchukua maamuzi ya kuongezea muda au kama haupo tena duniani itafutwa.
| Andika barua pepe au namba ya simu |
| Andika muda wa katizo la akaunti yako |
| Andika namba za jamaa ambao watapewa taarifa kabla akaunti yako kufutwa |
| Kubali mfumo kuweza kufuta akaunti yako pindi muda ulioweka ukifika |
About Admin MC3
This is dummy text. It is not meant to be read. Accordingly, it is difficult to figure out when to end it. But then, this is dummy text. It is not meant to be read. Period.


ConversionConversion EmoticonEmoticon