adsense

Biashara na Mahusiano Katika jamii inayo kuzunguka.

                                                                               
 Biashara na mahusiano katika jamii inayokuzunguka/ inayotuzunguka, wengi wetu tumekuwa tukijihusisha na ujasiria mali ama biashara ndogo ndogo za kati na zile kubwa kubwa ambazo zote kwa ujumla wake huitwa ujasiria mali, ingawa ujasiria mali wa kweli ni pamoja na kuletea ama kuja na kitu kipya ama kuongeza thamani ya kile kilichopo sokoni. Kuwa na bidhaa sokoni ni jambo moja na kuuuza ni jambo jingine, ama kuwa na masoko ya kile unacho zalisha ni jambo jingine hapa ndipo mahalli ambapo wengi wetu tuna shindwa kutofautisha.
     Unaweza kuta mtu ama watu wanazalisha bidhaa ya aina flani ambayo ni bora katika jamii inayo wazunguka, lakini mtu/watu wakashindwa/shindwa fikia malengo walio jiwekea ama matarajio yao katika biashara husika kwa sababu tu wamekosa soko/masoko ya kile wanacho zalisha.

NIDHAMU KATIKA UJASIRIAMALI;

   Katika shughuli nzima ya ujasiriamali, kitu cha kwanza kuzingatia ni nidhamu ya kile ama katika kile unacho kifanya , kuwa na nidhamu katika jambo fulani ni daraja litakalo kuvusha wewe ili kufikia kile kinacho itwa  mafanikio.
         Pengine unazalisha bidhaa bora sana katika  ujasiria mali  wako, lakini ukienda  sokoni  zinakosa wateja, pengine unatumia nguvu kubwa sana kuutangazia umma aina ya bidhaa zako na ubora wake kwa ujumla, lakini bado idadi ya mauzo iko chini kulinganisha na nguvu ya uzalishaji.
Inawezekana unajiuliza maswali mengi sana  ambayo huna majibu nayo katika kichwa chako, pengine ume ajiri sales manager uliye amini ni mtu bora na makini ambaye atakusaidia kukuza biashara yako kutoka hapo ilipo na kwenda kule unapo hitaji. Lakini je! umewahi kujiuliza kuhusu nidhamu yako na wafanyakazi wako dhidi ya jamii inayo wazunguka?.

   Inawezekana ni kweli bidhaa zenu ni bora na zenye viwango stahiki, lakini watu wanapo weka oda  kwenu mna deliver nje ya muda, na hata mkichelewa ku deliver hamuombi radhi kwa usumbufu. Inawezekana mahusiano yenu na wateja ni ya kiwango chini sana katika biashara, je ni kwa namna gani mna boresha mahusiano haya?, inawezekana ukawa mtu uliye na mahusiano mazuri na wateja wako, lakini wafanyakazi ama watu wanao kusaidia kazi hawana mahusiano yenye afya na jamii husika. Hatua ya kwanza katika ujasiria mali ni  kujenga nidhanu baina yako na jamii, wateja, na wafanyakazi wako.

HESHIMA KATIKA UJASIRIAMALI;

Katika wigo wa ujasiria mali HESHIMA ni msingi miongoni mwa misingi ya ujasiria mali, tabia zako dhidi ya jamii inayo kuzunguka ni silaha bora ya wewe kufanikiwa, lakini  tabia hiyo hiyo  ikiwa mbovu dhidi ya jamii yako, inaweza ikawa moja ya sababu ya wewe ku feli katika ujasiria mali ulio uanzisha. Ujasiria mali  ni pamoja na kuwa heshimu wakubwa kwa wadogo, kuheshimu  wafanyakazi ama watu unao saidiana nao kazi pamoja na kwamba una walipa kwa kile wanacho kifanya, ila bado wanastahiki heshima toka kwako maana wao pia ni binaadamu.
  Kuheshimu mawazo ya wengine katika kile unacho kifanya kutakupa matokeo chanya na hasi kwa ujumla wake, pia katika kuheshimu mawazo ya wengine waweza kuyachukua yale yanayo faa na kuyafanyia kazi.

      Heshima ni pamoja na kuwa heshimu washindani wako kibiashara, moja ya maeneo muhumu ambyo wajasiria mali  wengi huwa wana feli ni pamoja na kuto toa  heshima ya kutosha kwa washindani wao, bila hawa wewe huwezi ku mantain uzalishaji ulio bora, huwezi kuja na wazo jipya dhidi yao maana huna changamoto inayo kufanya wewe kufikiri zaidi yaa.
       Hivyo yakupasa kujijengea utamaduni wa kuwa heshimu  watu wa rika zote katika jamii inayo kuzunguka.


                                     https://web.facebook.com/Mwarokamainvestment/


KUJITANGAZA  KATIKA UJASIRIAMALI;


Uzalishaji wako si kitu mbele ya jamii ikiwa huiambii jamii nini unafanya, biashara ni matangazo makampuni makubwa yenye zaidi ya karne moja hapa ulimwenguni bado yanaamini katika kujitangaza je! we ni nani hata ukadharau katika kuitangangaza biashara yako. Unaweza kuwa unazalisha bidhaa iliyo na ubora stahiki, lakini huiambii jamii juu ya uzalishaji wako, huitangazii bidhaa yako katika njia zinazo faa,  huiweki bidhaa yako katika ramani stahiki.
    Lazima uiambie jamii wewe ni nani, uko wapi, na unafanya nini, na kile unacho kifanya kina manufaa haya na haya katika jamii ikiwa mtaniunga mkono. Unaweza kuwa mwandishi mzuri sana wa makala, lakini kila ukiandika una acha maandiko yako katika makratasi kabatini mwako, unaweza kuwa una kipaji cha ualimu katika mambo mbalimbali  lakini tutajua vipi ikiwa hutoki hadharani kutufundisha juuu ya kile unacho kijua?.

Unaweza kujitangaza katika jamii inayo kuzunguka kwa kujitoleaa katika shughuli za maendeleo, hii ni njia nzuri na bora ya kuingia katika mioyo ya watu na wateja wako, kwa kujitolea kwako we na kampuni yako kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo kwenye jamii huusika kuta pelekea jamii ukutambue,ukuthamini, ukujari, na kuheshimu kile unacho zalisha, maana yake tayari umekwisha ingia kwenye mioyo ya watu. Hapa ndipo tunapo ita mafanikio ya kweli huja kwa wakati ulio bora zaidi, jiandae kukua na kustawi kiuchumi baada ya hili.



Mwisho nisema karibuni sana katika blog yetu kwa habari makala mabli mbali zinahusu ujasiria mali, pia msisahau ku SHARE na wengine juu ya maandiko/makala zetu ili tuweze kutengeneza familia kuubwa katika ujasiria mali.

#i_see_all_of_you_at_the_top


Previous
Next Post »