Anasema kila alipokuwa ananyanyaswa na wateja wabaguzi waliokuwa wanakuja katika duka ndivyo ambavyo alikuwa anazidi kupata hamasa ya kufanya kazi zaidi kwa bidii na kufukia malengo ambayo anayo kwenye maisha yake.Siku moja alifanya maamuzi kuwa ni lazima afanye kazi kaw bidii ili siku moja aje kuwa na uhuru wa kifedha.Anasema kwa sababu alikuwa hata ana akaunti ya kupeleka fedha,aliamua kuwa kila wakati atakuwa anaweka fedha ambayo anaipata kwenye bahasha yake na baadaye mwisho wa mwaka aliamaua kuitumia kama ndio mtaji wake wa kwanza.Leo hii ana utajiri wa zaidi ya milioni 100 na shida zote zilizokuwa zinamkabili zimeshaisha.
Maisha yake yanatoa mafunzo kadhaa kwa kila ambaye anatafuta mafanikio kwenye maisha yake.Jambo la kwanza ni kuanza pale ulipo kwa kile ulichonacho na vile unavyoweza.Usikubali kuendelea kusubiria wakati kuna ambacho uanweza kufanya kwa sasa kwa kile ulichonacho.Ingawa alikuwa na ndoto kubwa sana za maisha yake,alikubali kujishughulisha na jambo dogo ambalo lingemsaidia kumsogeza kwenye hatua inayofuata ya maisha yake.Usikubali kuzuiwa kupiga hatua kufuata unachokiamini kwa sababu haujapata kikubwa unachotaka,anza na kidogo unachoweza kwa sasa.
Jambo la pili la kuliangalia hapa ni kuwa,hakuruhusu watu waliokuwa wanamdharau kwa kuwa sio mmarekani kumfanya akate tamaa,bali aliifanya kuwa ni motisha kwenye maisha yake na kuelekea kwenye ndoto yake kubwa.Kila kitu na kila mtu ambaye anakuambia ama kukuonyesha wewe si kitu ama hautasonga mbele,tumia hiyo kama motisha ya kukusaidia kusonga mbele zaidi na sio kukukatisha tamaa ya kusogea.
Jambo la tatu na la mwisho ni jinsi ambavyo aliweza kujiwekea nidhamu ya kuweka kidogokidogo hadi kufikia lengo alilokuwa nalo.Nawe usidharau kile kidogo ambacho unacho mkononi kwa sasa,unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa kwa kila kidogo ulichonacho uanweka kidogokidogo hadi kufikia kiwango kikubwa uanchokitaka.Kila kinachopita katika mikono yako ni mbegu unayotakiwa kuikuza ili izae na kuwa kubwa zaidi.Usidharau mshahara ulionao leo,usidharau faida unayopata leo,usidharau kidogo unachopata,tafuta namna ya kukitumia na kukizalisha ili kikusaidie baadaye kutimiza malengo yako.
See You At The Top
#TIMIZAMALENGOYAKO

ConversionConversion EmoticonEmoticon