adsense

MJASIRIAMALI WA KIFO ALIPOKUFA.


Na Francis Daudi.
Inashtua kidogo lakini ndivyo ilivyoripotiwa mwaka, 1888 alipofariki Ludvig ambaye ni mdogo wa Afred Nobel(Muasisi wa tunzo za Nobel). Lakini magazeti hayakuripoti kifo hicho kumrejelea Ludvig bali kaka yake, Nobel. Wengi hawamfahamu kabisa Nobel na maisha yake, Huyu ni mwanasayansi ambaye aligundua baruti. 

Alfred Bernhard Nobel alikuwa mswidishi ambaye alifanya majaribio mengi katika masuala ya vilipuzi. Mwaka 1867 aligundua baruti ambazo zimetumika katika kupasua miamba wakati wa ujenzi wa madaraja na barabara, Lakini pia baruti zilitumika kubomoa majengo yaliyokosewa.
Hii ilimfanya kuwa tajiri mkubwa kwani serikali za mataifa makubwa ziliitaji baruti katika shughuli za ujenzi wa miundo mbinu na uchimbaji wa madini. Pia baruti zilionekana kama njia rahisi ya watu kujiua au kufanya uhalifu mkubwa. Vilipuzi vilitumika zaidi wakati wa vita kati ya Uhispania na marekani ‘Spanish-American War’ na kusababisha vifo vingi zaidi.

Mwaka 1888, kulitokea mlipuko mkubwa katika maabara zilizomilikiwa na Alfred Nobel, walifariki watu kadhaa akiwemo mdogo wake Ludvig na Emil. Baada ya mlipuko huo mji wa Stockholm ulipiga marufuku majaribio yoyote ya baruti ndani ya mji. Hilo halikuwa jambo kubwa, Lakini tukio lililoshtua ni kutaarifiwa kimakosa kuwa aliyefariki katika mlipuko huo ni Nobel mwenyewe na watu wengine.
Magazeti kadhaa yaliripoti kwa pamoja kuwa ‘Mjasiriamali wa kifo amefariki’ gazeti la ufaransa lilikolezea kuwa "Le marchand de la mort est mort," au kwa kiingereza "the merchant of death is dead." Hii ilimshtua sana Nobel kwani hakuwa anajua jinsi watu walivyomchukulia. Alijihisi ni mtu mwenye heshima na kupendwa mno kutokana na kazi zake. Lakini hakuweza kujua nini kitaandikwa baada ya kifo chake, toka hapo alijiona ni mtu asiyefaa nah ii ilimsababisha kutokuwa na mke wala mtoto mpaka kifo chake.

Alibadili mfumo wa maisha yake na kabla ya kifo chake, aliandika wosia kuwa mali zake zote zitumike katika kampeni za kuleta amani duniani, pia zisaidie kusambaza upendo na kuboresha hali za watu kupitia taaluma. Tuzo za Nobel zilianzishwa kupitia fedha alizoziacha na viwanda vya baruti katika karibu nchi zote za ulaya. Nobel ni mmoja kati ya matajiri waliopata kutokea katika ulimwengu huu.
Unajua jinsi matendo yako yanavyochukuliwa na wengine? Je sura unazooneshwa na watu ndio mioyo yao ilivyo? Jipange kusambaza upendo na amani daima. Barikiwa
Francis Daudi
Mdau wa maendeleo.
Previous
Next Post »